SAFARI YA KWANZA SHULENI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Baraka alikuwa mtoto wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Upendo. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda shule na alikuwa na furaha lakini pia alikuwa na hofu kidogo. Alikuwa amesikia hadithi nyingi kuhusu shule kutoka kwa watoto wakubwa.

Asubuhi moja mama yake alimwamsha mapema. Akamvalisha sare yake mpya ya shule na kumfungia begi lake. Njiani kuelekea shuleni Baraka alimshika mama yake mkono kwa nguvu.

Alipofika shuleni aliona watoto wengi wakicheza na wengine wakilia. Mwalimu wao Bi Rehema aliwapokea kwa tabasamu na kuanza kuwafundisha wimbo mfupi. Taratibu Baraka akaanza kujisikia vizuri.

Wakati wa mapumziko Baraka alikosa chakula chake. Alianza kulia kimya kimya. Mtoto mmoja aitwaye Musa alimwona na akamgawia mkate wake. Tangu siku hiyo Baraka alipenda shule na alipata rafiki mpya.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments