NYANI NA NDIZI TAMU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na nyani mmoja aliyeitwa Koki. Koki alipenda sana kula ndizi lakini alikuwa mchoyo. Hakupenda kugawana chakula na wengine.

Siku moja Koki alipata mgomba wenye ndizi nyingi sana. Akafurahi na kuanza kula peke yake. Rafiki zake sungura, kasa na ndege wakamwomba awape hata ndizi moja.

Lakini Koki akasema “Hizi ni zangu peke yangu sitaki kugawana na nyinyi!”

Alipokuwa anaendelea kula siku hadi siku ndizi zikaanza kuoza kwa sababu alikuwa na nyingi kuliko alivyoweza kula. Ndizi nyingi zikaharibika.

Baadaye Koki akahisi njaa tena lakini ndizi zilikuwa zimekwisha. Alijuta sana akaenda kwa rafiki zake na kuomba msamaha. Rafiki zake wakamsamehe na wakamfundisha kuwa kugawana huleta furaha.

Tangu siku hiyo Koki akawa nyani mkarimu na mwenye marafiki wengi kushinda kipindi cha nyuma.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments