Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Neema alikuwa msichana wa darasa la nne aliyeishi na wazazi wake kijijini. Kila asubuhi aliamka mapema kufagia uwanja,kuchota maji na baada ya kazi kumalizika huenda shuleni.
Siku moja shuleni mwalimu alitangaza kuwa “Kesho kila mwanafunzi aje na daftari jipya.”
Neema alihuzunika kwa sababu wazazi wake hawakuwa na pesa za kununua daftari jipya. Usiku alimwambia mama yake. Mama akamkumbatia na kusema.
“Kesho nenda shule tutatafuta suluhisho la kununulia daftari jipya.”
Kesho yake Neema alienda shule na daftari lake la zamani. Alimwambia mwalimu ukweli. Mwalimu alitabasamu na kusema
“Asante kwa kusema ukweli. Uaminifu wako ni muhimu kuliko daftari.”
Baadaye mwalimu alimpa daftari jipya kutoka shuleni. Neema alifurahi sana na akaendelea kusoma kwa bidii.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpeg)


Post a Comment