Mwanakwetukids
Amani ni msichana wa miaka 10 anayeishi Iringa. Kila siku baada ya shule anasaidia mama yake kuandaa chakula na kuangalia wadogo wake. Lakini licha ya kazi nyingi Amani anapenda kusoma. Shule yake ni ndogo na mara nyingi haina vitabu vya kutosha.
Siku moja Amani alipata kitabu cha hadithi kilichoachwa kwenye mtaa. Alifurahi sana lakini akatambua kitabu hicho ni cha mtaa na wengine wanaweza kuhitaji pia. Alifikiri kwa muda kisha akachukua kitabu hicho na kwenda nacho shuleni na kuanza kusoma wakati wa mapumziko.
Marafiki zake waliona na kumsaidia kusoma. Walijifunza pamoja maneno mapya na kuzungumza kuhusu hadithi. Amani alifurahi lakini pia alijua kuwa shuleni au mitaani kila mtoto anapaswa kupata nafasi ya kujifunza.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment