Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika msitu mkubwa aliishi simba mwenye nguvu sana. Wanyama wote walimwogopa. Karibu naye aliishi panya mdogo aliyekuwa mcheshi na mkarimu.
Siku moja simba alimkamata panya na kusema “Leo nitakula wewe!” Panya akaomba
“Tafadhali usinile. Nikiachia huru siku moja nitakusaidia.”
Simba akacheka sana “Wewe mdogo utanisaidia mimi? Hilo haliwezekani!”
Lakini kwa sababu simba alikuwa na moyo mwema alimwachia panya aende.
Baada ya siku chache simba alinasa katika mtego wa wawindaji. Alijaribu kujitoa lakini alishindwa. Akaanza kulia kwa sauti kubwa.
Panya akasikia kilio Akakimbia haraka akaanza kung’ata kamba za mtego kwa meno yake madogo. Baada ya muda simba akaachiliwa huru!
Simba akasema kwa mshangao “Asante sana rafiki yangu! Nilidhani huwezi kunisaidia lakini nimekosea.”Panya akatabasamu
“Usidharau mdogo kila mtu ana uwezo wake.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment