Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Liam alikuwa mvulana wa miaka kumi aliyeishi na wazazi wake katika mtaa wa kawaida karibu na shule ya msingi. Hakukuwa na mambo ya ajabu sana katika maisha yake ila jambo moja lililomtofautisha na watoto wengine: Liam hakuwahi kukata tamaa.
Kila asubuhi Liam aliamka mapema. Alijipanga mwenyewe akavaa sare yake ya shule kisha akamsaidia mama yake kuchota maji au kufagia uwanja. Baada ya hapo alichukua begi lake na kuanza safari ya kwenda shule kwa miguu.
Njiani alikutana na changamoto nyingi. Wakati wa mvua barabara ilikuwa na matope. Wakati mwingine jua lilikuwa kali sana. Lakini Liam aliendelea kutembea akijua elimu ni muhimu kwa maisha yake ya baadaye.
Siku moja alipofika shuleni aligundua kuwa kalamu yake pekee ilikuwa imeisha wino. Alisikitika sana kwa sababu siku hiyo walikuwa na jaribio darasani. Alikaa kimya akifikiri nini cha kufanya.
Rafiki yake Noah alimwona akiwa na huzuni. Akamkaribia na kusema
“Liam tumia kalamu yangu leo.” Liam alifurahi sana. Baada ya jaribio alimshukuru Noah kwa moyo wote. Tukio hilo lilimfundisha kuwa kusaidiana ni jambo muhimu sana.
Jioni, Liam aliporudi nyumbani, alimwambia mama yake kilichotokea. Mama yake akamwambia
“Mtoto wangu unapojitahidi na kuwa mwema msaada huja pale unapouhitaji.”
Kuanzia siku hiyo Liam alizidi kuwa mwanafunzi mwenye bidii msaidizi nyumbani na rafiki mzuri kwa wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
i@gmail.com
0653903872



Post a Comment