KUKU ALIYETAKA KURUKA ANGANI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kuku mdogo aliyeitwa Kiki alikuwa na ndoto kubwa sana alitaka kuruka juu kama ndege wengine. Kila siku aliwaona tai wakiruka juu angani na alitamani kufanya hivyo pia. Alisema mara nyingi “Siku moja nitaruka hadi mawinguni!”

Bata alimcheka na kumwambia kuwa kuku hawezi kuruka juu hivyo. Lakini Kiki hakukata tamaa. Aliamua kujaribu mwenyewe.

Siku ya kwanza alipanda juu ya jiwe akaruka… akaanguka. Siku ya pili alipanda juu ya uzio akaruka tena… akaanguka tena. Siku ya tatu alipanda juu ya paa la banda akaruka na akaanguka kwenye nyasi laini.

Baada ya kuanguka mara nyingi alikaa kimya akiwaza. Akasema polepole “Labda siwezi kuruka juu sana lakini naweza kufanya kitu kingine.”

Kesho yake aliamka mapema sana kuliko kawaida. Akapiga kelele “Kooo! Kooo! Kumepambazuka!” Wanyama wote wakaamka mapema mkulima akaenda shambani kwa wakati na ng’ombe wakapata malisho mapema. Kila mtu akafurahi sana.

Bata akamwambia “Huendi angani lakini unatupa mwanzo mzuri wa siku.” Kiki akatabasamu na kufurahi.Hatimaye aligundua jambo muhimu si lazima uwe kama wengine ili uwe wa muhimu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments