KOBE NA NDEGE WAWILI


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na Kobe aliyeishi karibu na ziwa. Kobe alikuwa mzuri wa moyo lakini alipenda sana kuzungumza. Karibu na ziwa hilo waliishi ndege wawili rafiki.

Siku moja ukame mkubwa ulitokea. Ziwa likaanza kukauka na wanyama wakatafuta mahali pengine pa kuishi. Ndege wakaamua kuhama kwenda mbali ambako kulikuwa na maji.

Wakamwambia Kobe “Rafiki yetu tungependa uende nasi lakini hutakiwi kuzungumza ukiwa njiani.”

Kobe akakubali. Ndege wakabeba fimbo Kobe akauma katikati ya fimbo na ndege wakaruka.


Walipokuwa angani watu wakaona na kusema.

“Angalieni! Kobe anaruka!” Kobe aliposikia hivyo alitaka kujibu akafungua mdomo wake… akaanguka chini.

Kwa bahati nzuri aliangukia majani laini na hakuumia sana.

Tangu siku hiyo Kobe alijifunza somo muhimu si kila wakati kuzungumza ni vizuri.

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments