KIVULI CHA DARASA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Katika Shule ya Msingi Mwangaza kulikuwa na darasa moja la zamani lililokuwa halitumiki tena. Watoto walikuwa wakisema kuwa darasa hilo lina kivuli cha ajabu kinachoonekana jioni.

Mwanafunzi mmoja aitwaye Asia hakupenda kuamini maneno ya kuogopesha. Alikuwa jasiri sana. Siku moja alichelewa kutoka shuleni baada ya kusafisha ubao. Ilipofika jioni shule ilikuwa kimya sana. Hakukuwa na kelele za watoto wala sauti za walimu.

Asia alipokuwa akipita karibu na lile darasa la zamani alisikia sauti ya mtu akigonga dirisha Gonga… gonga… gonga…

Moyo wake ulianza kudunda. Alisimama. Ghafla akaona kivuli cheusi kikisogea ukutani. Kivuli kile kilionekana kama mtu lakini hakikuwa na uso.

Asia alitaka kukimbia lakini miguu yake ilitetemeka. Kivuli kile kilisema kwa sauti ya chini

“Rudi… rudi… usibaki hapa…”


Kwa hofu kubwa Asia alikimbia mpaka nyumbani bila kugeuka nyuma. Usiku huo hakulala vizuri.

Kesho yake alimwambia mwalimu wake. Mwalimu alitabasamu na kusema

“Darasa lile lina bundi wanaoishi juu ya paa. Sauti na vivuli ni vyao.”

Asia alijifunza kuwa wakati mwingine hofu huja kwa sababu ya kutokujua. Lakini tangu siku hiyo hakuwahi kuchelewa shuleni tena.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments