Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika shamba moja waliishi wanyama wengi kwa amani. Kila mmoja alikuwa na kazi yake na kiongozi wao alikuwa mbwa mzee mwenye hekima.
Siku moja sungura mdogo Kito alitamani kuwa kiongozi. Alisema
“Mimi nakimbia haraka kuliko wote kwa hiyo ninafaa kuwa mkuu!”
Mbwa hakubishana. Akasema “Sawa utakuwa kiongozi kwa siku moja.”
Kesho yake Kito alitoa amri “Kuku wafanye kazi zaidi! Ng’ombe walime bila kupumzika!”
Baada ya muda wanyama walichoka sana. Waliposhindwa hata kumfukuza mbweha aliyekuja shambani Mbwa aliwasaidia na kupanga kazi vizuri mpaka kila mmoja akapata nguvu tena.
Jioni Kito aliona aibu. Akasema “Nimejifunza kiongozi si yule anayetoa amri nyingi bali anayejali wengine.” Mbwa akatabasamu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment