JE, MTOTO AKISUKWA AKIWA MDOGO ANAKOMAA KICHWA?

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kumekuwa na imani katika jamii kwamba mtoto akianza kusukwa nywele akiwa mdogo basi kichwa chake kinakoma au hakikui vizuri. Wazazi na walezi wengi wamekuwa wakiamini jambo hili na kuwazuia watoto wao kusukwa mapema.

Hakuna ushahidi wa kitabibu unaoonrsha kuwa kusuka nywele za mtoto husababisha kichwa kukoma kukua. Ukuaji wa kichwa cha mtoto hutegemea zaidi ukuaji wa ubongo, lishe bora na afya ya mtoto kwa ujumla siiyo kusuka nywele. Kichwa cha mtoto hukua kulingana na umri wake na maumbile aliyorithi kutoka kwa wazazi wake.

Hata hivyo kusuka nywele kwa mtindo mkali sana kunaweza kusababisha maumivu ya kichwa au kuharibu ngozi ya kichwa cha mtoto. Hii inaweza kusababisha vidonda au nywele kung’oka lakini haimaanishi kuwa kichwa kinakoma. Ndiyo maana wataalamu wa afya wanashauri watoto wasukwe kwa upole au waachwe na nywele za asili wanapokuwa wadogo.

Kwa hiyo naweza kusema kuwa imani ya kwamba mtoto akisukwa mdogo anakomaa kichwa si ya kweli kisayansi. Kilicho muhimu ni kumtunza mtoto kwa kumpatia lishe bora huduma za afya na usafi wa mwili. Pia wazazi wanapaswa kuepuka mitindo ya nywele inayoumiza watoto.

Kusuka nywele za mtoto akiwa mdogo hakukomazi kichwa bali kinachohitajika ni uangalizi mzuri na matumizi ya elimu sahihi badala ya kuamini dhana zisizo na msingi wa kisayansi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments