Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kevin alikuwa mtoto aliyeishi mjini Dar es Salaam katika mtaa wa Buguruni. Alisoma Shule ya Msingi Amani. Kevin alikuwa mchoyo na mroho sana. Hakupenda kushirikiana chochote na wenzake hata kama walikuwa na njaa.
Kila asubuhi mama yake alimwandalia bakuli la chakula lenye wali kuku au biskuti. Shuleni wakati wa mapumziko Kevin alikaa peke yake chini ya mti. Alipofungua sanduku lake aliwatazama wenzake kwa macho ya kujivunia.
Watoto walipomwomba Kevin alikuwa akijibu “Hiki ni chakula changu. Kila mtu ale chake.”
Siku moj mama yake Kevin aliumwa na hakuweza kwenda kazini. Siku hiyo Kevin alienda shule bila chakula. Alipofika mapumziko njaa ilimzidi. Aliwaangalia wenzake wakila lakini hakuna aliyemkaribia. Wote walikumbuka tabia yake ya uchoyo.
Kevin alihisi huzuni sana. Machozi yakamtoka. Baada ya muda rafiki mmoja aitwaye Asha alimletea kipande kidogo cha mkate na kusema
“Chukua hata kidogo.” Kevin alishangaa na akaona aibu. Alitambua kosa lake. Tangu siku hiyo Kevin alianza kushirikiana chakula chake na wenzake. Akaacha uroho na uchoyo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment