Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika kijiji cha Mwembe aliishi msichana mdogo aliyeitwa Asha. Asha alipenda sana maua. Kila asubuhi alikuwa akiyamwagilia bustani yao.
Siku moja alipokuwa akitembea msituni aliona ua moja la ajabu likiwa linang’aa kama dhahabu. Alilishangaa sana na kulichukua kwa uangalifu.
Alipolipeleka nyumbani alilipanda kwenye bustani. Kesho yake ua lile lilikua haraka sana na kutoa matunda matamu kuliko yote kijijini!
Watu wakasikia habari hizo. Walianza kuja kuomba Asha awape matunda. Asha hakuwanyima mtu yeyote. Aliwapa wote kwa moyo wa upendo.
Lakini kijana mmoja mwenye tamaa alitaka kulichukua ua lile peke yake. Usiku alienda kuling’oa. Lakini alipopanda kuling’oa ua lile likanyauka na kupotea.
Asubuhi yakeAsha alikuta ua limekufa. Alisikitika sana. Lakini alikumbuka kuwa alikuwa tayari ameshawapa watu wengi furaha.
Tangu siku hiyo Asha alijifunza kuwa Mema yakishirikishwa hudumu lakini tamaa huharibu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment