MBWA MTANASHATI

 

Emakulata Msafiri

Katika kijiji cha Mtakuja kulikua na mbwa mmoja anayeitwa Bula. Bula alipenda sana kuvaa Lakini siku moja akaamua kuvaa miwani ya bosi wake.

Akiwa amevaa miwani kubwa kuliko uso wake Bula akaenda sokoni. Watu wote wakaanza kucheka.

"Mbwa gani huyu anavaa miwani kama mzee wa baraza?" mtu mmoja akasema.

Bula hakujali. Alijiona anapendeza sana. Bula hakukata tamaa. Akaingia kwa fundi baiskeli.

"Nataka baiskeli irekebishwe!"Fundi akamwambia:"Lakini hii ni baiskeli ya paka, si yako!"

Bula akajibu: "Siwezi kuona vizuri, labda ni miwani ndiyo inanidanganya."

Hatimaye Bula akachoka kutembea huku akionekana kama mzee wa harusi. Alirudi nyumbani, akaiweka miwani chini, na kusema:

"Kuanzia leo sitavaa tena miwani bila sababu. Dunia inaonekana ya ajabu sana!"



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments