Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika nyumba moja ya kupanga mjini wapangaji walikuwa wakiishi kama watu wasiowafahamu. Kila familia ilikuwa na shughuli zake na wengi hawakujali yanayotokea kwa majirani zao.
Usiku mmoja mvua kubwa ilinyesha huku upepo mkali ukivuma. Katika moja ya nyumba hizo mwanamke aliyekuwa akiishi na watoto wake wawili aliteleza bafuni na kushindwa kuinuka kutokana na maumivu.
Watoto wake walijaribu kuita msaada lakini walihofia kusumbua majirani kwa sababu hawakuwa na mazoea ya kuzungumza nao.
Mmoja wa watoto alikumbuka kuwa jirani yao alikuwa amewahi kuwaambia wasisite kuomba msaada wanapokuwa na shida. Alitoka nje na kugonga mlango wa jirani kwa nguvu.
Jirani alipoelewa kilichotokea aliwaita wapangaji wengine. Kwa pamoja walimsaidia mwanamke huyo kufikishwa hospitalini.
Baada ya tukio hilo wapangaji walianza kujuana, kubadilishana mawasiliano na kusaidiana katika changamoto mbalimbali.
Mlango ambao zamani ulifungwa kila mtu alipoingia kwake sasa ulikuwa mwanzo wa ujirani wenye mshikamano.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment