SIMU ILIYOMFANYA AANZE KUJITENGA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Kila alipofika nyumbani kutoka shule kitu cha kwanza alichotafuta kilikuwa simu.

Alikuwa amezoea kukaa nayo hadi usiku. Kazi za shule alizifanya kwa haraka, chakula alikula huku akiangalia video na wakati mwingine alilala akiwa bado anashikilia simu.

Mwanzoni hakukuwa na mtu aliyeliona tatizo hilo.

Lakini baada ya muda mwalimu alianza kugundua kwamba mtoto huyo alikuwa akikaa kimya darasani. Kazi zake zilianza kuchelewa na alishindwa kuzingatia masomo kama zamani.

Hata marafiki zake walipojaribu kumshirikisha katika mazungumzo mara nyingi aliwaambia alikuwa busy kwenye simu.


Siku moja mwalimu aliwakabidhi wanafunzi kazi ya kufanya kwa makundi. Kundi lake lilipomaliza aligundua kuwa hakuelewa sehemu kubwa ya kazi kwa sababu alikuwa hajafuatilia maelekezo.

Aliporudi nyumbani alikaa na mzazi wake na kueleza kilichokuwa kinamsumbua.

Hakutakiwa kuacha simu kabisa. Alisaidiwa kuweka muda maalumu wa kutumia simu, muda wa kusoma, kula na kulala.

Baada ya wiki kadhaa alianza kubadilika. Alianza kumaliza kazi zake kwa wakati, kuzungumza zaidi na familia yake na kushiriki vizuri darasani.

Aligundua kuwa tatizo halikuwa simu yenyewe bali kutokujua kuitumia kwa kiasi.




emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments