Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kwa muda mrefu wanafunzi wa shule moja walikuwa wakiacha mabomba ya maji wazi baada ya kunawa mikono. Wengine walikuwa wakicheza kwa kurushiana maji bila kujali kiasi kilichokuwa kinapotea.
Siku moja asubuhi wanafunzi walipofika shuleni walikuta hakuna maji yaliyokuwa yakitoka kwenye mabomba. Walilazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji ya kunawa mikono baada ya kutumia vyoo.
Mwalimu aliwaeleza kuwa maji yalikuwa yameisha kwenye tenki kwa sababu yalitumika vibaya kwa siku kadhaa. Hali hiyo iliwafanya wanafunzi watambue kuwa tabia yao ilikuwa imewaathiri wao wenyewe.
Walipendekeza kuweka mabango karibu na mabomba yenye ujumbe wa kuhimiza matumizi sahihi ya maji. Pia walikubaliana kuhakikisha mabomba yanafungwa baada ya matumizi na kutoa taarifa haraka yanapovuja.
Baada ya siku kadhaa shule ilianza kufuatilia matumizi ya maji kwa umakini zaidi. Wanafunzi walijifunza kuwa rasilimali muhimu kama maji zinahitaji kutumiwa kwa uangalifu ili ziweze kuwatosha wote.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment