WATOTO ZANZIBAR WAHAMASISHWA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA ELIMU

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Watoto wa Zanzibar wamehamasishwa kutumia teknolojia katika kujifunza ili kuboresha ufaulu wao na kuwaandaa kwa mahitaji ya dunia ya kidijitali yamesemwa hayo siku ya julai 8,2026

Hatua hiyo ilisisitizwa na viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakati wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa programu za elimu ya kidijitali katika shule mbalimbali visiwani Zanzibar. Viongozi hao walisema matumizi ya vifaa vya kisasa vya TEHAMA yatasaidia watoto kujifunza kwa ufanisi zaidi na kuongeza ubunifu wao.

Walimu walieleza kuwa matumizi ya kompyuta na teknolojia nyingine za kisasa yameongeza hamasa ya watoto darasani na kuwasaidia kuelewa masomo kwa urahisi. Wazazi pia walikaribisha hatua hiyo wakisema itawajengea watoto ujuzi muhimu kwa maisha na ajira za baadaye.

Programu hiyo inalenga kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia huku shule zikiendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa kutumia vifaa vya kidijitali.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872





0/Post a Comment/Comments