Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limezitaka serikali, wazazi, walimu na jamii kuendelea kushirikiana kulinda haki za watoto na kuhakikisha wanapata elimu bora, huduma za afya na mazingira salama ya kukua.
Ujumbe huo ulitolewa jijini Dodoma siku ya jumatano Julai8,2026 ukisisitiza kuwa kila mtoto anapaswa kulindwa dhidi ya ukatili, unyanyasaji, ajira za watoto na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha maendeleo yake.
UNICEF ilieleza kuwa uwekezaji katika watoto ni msingi wa maendeleo endelevu ya Tanzania hivyo jamii nzima ina wajibu wa kuhakikisha watoto wanapata fursa sawa za kujifunza, kucheza na kukuza vipaji vyao.
Shirika hilo pia lilihimiza wadau wote kuendelea kushirikiana katika kutekeleza sera na programu zinazolenga kuboresha ustawi wa watoto ili waweze kukua katika mazingira salama na yenye kuwajengea maisha bora ya baadaye.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment