UAMINIFU NI UTAJIRI AMBAO HAUWEZI KUNUNULIWA KWA FEDHA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.

Siku moja mtoto mmoja alipokuwa akitoka shuleni aliona pochi ndogo ikiwa imelala kando ya barabara. Aliiinua na kuifungua ndani kulikuwa na fedha na kitambulisho cha mtu mzima.

Kwa muda mfupi alifikiria kuichukua lakini akakumbuka alichofundishwa na wazazi wake kwamba mali ya mtu mwingine si ya kwako.

Badala ya kwenda nayo nyumbani alikwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya serikali ya kijiji na kuikabidhi. Maafisa walitumia taarifa zilizokuwa kwenye kitambulisho kumpata mwenye pochi.

Baada ya muda mfupi mwenye pochi alifika akiwa na furaha kubwa. Alisema fedha zile zilikuwa za kulipia matibabu ya mtoto wake na alikuwa ameshakata tamaa ya kuzipata tena.

Aliwashukuru viongozi wa kijiji na akampongeza mtoto huyo kwa uaminifu wake. Habari hiyo ilienea shuleni na walimu walimtaja kama mfano wa kuigwa wakati wa mkutano wa asubuhi.

Mtoto huyo hakupata tu pongezi bali pia alijifunza kwamba kufanya jambo sahihi huleta heshima na amani ya moyo.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872




0/Post a Comment/Comments