Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.
Siku moja kulikuwa na mtoto aliyeishi na bibi yake katika kijiji kidogo. Kila asubuhi alimsaidia bibi kumwagilia bustani ya mboga.
Siku moja walipokuwa wakipalilia yule mtoto aliona kikapu kilichojaa mbegu mbalimbali. Alimuuliza bibi kwa nini unahifadhi mbegu nyingi hivi.
Bibi akatabasamu na kusema "Mbegu hizi ni maisha ya kesho tukizitunza leo tutapata chakula kesho".
Mtoto akachukua baadhi ya mbegu na kuzipanda kwenye sehemu ndogo ya bustani. Kila siku alimwagilia maji na kuondoa magugu. Baada ya wiki chache mimea ilianza kuchipua na kukua vizuri.
Msimu wa mavuno ulipofika bustani ilijaa mboga nyingi. Familia yao ilipata chakula cha kutosha na hata waliwapa majirani waliokuwa na uhitaji.
Mtoto alifurahi sana. Aligundua kuwa uvumilivu kazi ya bidii na kutunza vitu vidogo vinaweza kuleta matokeo makubwa.
Tangu siku hiyo hakuwahi kupoteza mbegu wala kupuuza kazi ya bustani. Alijifunza kwamba kila jambo kubwa huanza na hatua ndogo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment