MABADILIKO MAKUBWA HUANZA NA HATUA NDOGO

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kila siku wakati wa mapumziko watoto wengi walikuwa wakitupa vifungashio vya pipi na chupa za plastiki uwanjani. Baada ya muda mazingira ya shule yakawa machafu na baadhi ya wanafunzi wakaanza kuugua mara kwa mara.

Siku moja mtoto mmoja alisimama mbele ya darasa na kusema "Shule yetu ni nyumba yetu ya pili. Tukiitunza tutakuwa salama na wenye afya Ingawa baadhi ya wenzake walimcheka hakuvunjika moyo.

Alianza kuokota taka kila mwisho wa mapumziko na kuzitupa kwenye pipa. Polepole wanafunzi wengine walijiunga naye. Walimu waliona juhudi hizo na kuanzisha siku maalumu ya usafi kila Ijumaa.

Baada ya miezi michache shule ikawa safi zaidi kuliko ilivyowahi kuwa. Wageni waliotembelea shule hiyo waliisifu kwa mazingira yake mazuri na wanafunzi walijivunia kuona juhudi zao zimeleta mabadiliko.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments