Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.
Hapo zamani za kale msituni waliishi sungura mmoja aitwaye Kito na kasa mmoja aitwaye Tunu. Kito alikuwa na kasi sana lakini mara nyingi aliwacheka wanyama wengine kwa sababu walitembea polepole.
Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Mto ulifurika na mtoto wa ndege alikwama kwenye kichaka karibu na maji. Wanyama wengi waliogopa kumsaidia.
Kasa alitembea polepole hadi alipofika karibu na kichaka. Wakati huo Sungura Kito alikimbia haraka kuleta mzabibu mrefu. Kwa pamoja walivuta kichaka na kumwokoa mtoto wa ndege.
Mtoto wa ndege aliwashukuru sana. Wanyama wote walifurahi na kumpongeza Sungura kwa kutumia kasi yake kusaidia wengine na kumpongeza Kasa kwa uvumilivu na ujasiri wake.
Kuanzia siku hiyo sungura Kito aliacha kuwacheka wenzake. Alijifunza kwamba kila mmoja ana kipaji chake na wakishirikiana wanaweza kufanya mambo makubwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653902872



Post a Comment