Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja darasani kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya mwanafunzi mmoja. Wazazi wake walileta keki kubwa ili wanafunzi wote wale.
Mwalimu alianza kugawa vipande vya keki kwa kila mtoto. Kabla ya zamu yake kufika keki ilibaki na kipande kimoja tu.
Wakati huo kulikuwa na mtoto mwingine aliyekuwa ametoka hospitalini na alikuwa amechelewa kufika shuleni. Alipoingia darasani aliona wenzake wakila keki lakini hakusema chochote.
Mtoto aliyekuwa amebakiza kipande cha mwisho alisimama na kusema "Nitamwachia mwenzangu ale. Nitafurahi nikiona naye anatabasamu."
Mtoto aliyekuwa amechelewa alifurahi sana na akamshukuru.
Mwalimu alisema "Kushiriki si kuwa na vitu vingi bali ni kuwa na moyo wa kujali wengine".
Tangu siku hiyo wanafunzi walijifunza kwamba furaha huongezeka unaposhiriki na wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment