Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mtoto ni sehemu muhimu ya familia na anaweza kuwa chanzo cha
maendeleo ikiwa atapata malezi bora, elimu na mazingira yanayomwezesha kukuza
vipaji vyake. Ingawa mara nyingi wazazi huonekana kuwa nguzo kuu ya maendeleo
ya familia. Watoto pia huchangia kwa njia mbalimbali kama vile kufanya vizuri
shuleni, kuwa na nidhamu na kushiriki shughuli zinazokuza ustawi wa familia
(UNICEF, 1989).
Elimu ni njia mojawapo inayomwezesha mtoto kuchangia
maendeleo ya familia. Mtoto anayejituma katika masomo huongeza nafasi ya kupata
elimu ya juu na baadaye ajira au kujiajiri jambo ambalo linaweza kuinua hali ya
maisha ya familia yake. Pia mtoto mwenye maadili mema hujenga heshima ya
familia katika jamii na kuwa mfano mzuri kwa watoto wengine (UNESCO, 2021).
Aidha watoto wenye vipaji katika michezo, sanaa, muziki au ubunifu wanaweza kuitangaza familia yao na hata kupata fursa za kiuchumi. Hii inaonesha kuwa maendeleo ya familia hayategemei fedha pekee bali pia juhudi, maarifa na vipaji vya watoto vinavyokuzwa tangu wakiwa wadogo (UNICEF, 2021).
Kwa ujumla mtoto anaweza kuwa chanzo cha maendeleo ya
familia ikiwa atapatiwa haki zake za msingi, hasa elimu, afya na malezi bora.
Ushirikiano kati ya wazazi, shule na jamii ni muhimu katika kumwezesha mtoto
kutumia uwezo wake kwa manufaa ya familia na taifa (United Republic of
Tanzania, 2009).
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment