Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mtoto ana wajibu muhimu katika familia lakini uwezo wake wa kutambua na kutekeleza wajibu huo hutegemea umri wake, malezi anayopata na mazingira anayoishi. Familia ndiyo msingi wa kwanza unaomfundisha mtoto maadili, heshima, ushirikiano na uwajibikaji (UNICEF, 1989).
Baadhi ya wajibu wa mtoto katika familia ni kuwaheshimu wazazi na walezi, kutii maelekezo yanayolenga ustawi wake, kushiriki kazi ndogo za nyumbani kulingana na umri wake, kujituma katika masomo na kuishi kwa maadili mema. Mtoto anayetekeleza wajibu wake huchangia kujenga amani na mshikamano katika familia (UNICEF, 1989).
Hata hivyo si watoto wote wanaotambua wajibu wao ipasavyo. Ukosefu wa malezi bora, mawasiliano hafifu ndani ya familia na athari za mazingira au marafiki vinaweza kumfanya mtoto ashindwe kutimiza wajibu wake. Hivyo wazazi na walezi wanapaswa kutoa mwongozo unaofaa na kuwa mfano mzuri kwa watoto wao (UNICEF Tanzania, 2024).
Kwa ujumla mtoto anaweza kutambua na kutekeleza wajibu wake katika familia ikiwa atapata malezi bora, elimu ya maadili na mwongozo sahihi kutoka kwa wazazi, walezi na jamii. Hii humsaidia kukua akiwa mtu mwenye nidhamu, uwajibikaji na mchango chanya kwa familia na jamii.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment