NGUVU YA UPENDO KATIKA MAISHA YA MTOTO

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Upendo ni jambo muhimu sana katika maisha ya kila mtoto. Mtoto anahitaji kupendwa ili akue vizuri kimwili, kiakili na kihisia. Upendo humfanya mtoto ajisikie salama mwenye thamani na mwenye furaha katika maisha yake ya kila siku.

Wazazi na walezi wana jukumu kubwa la kuonyesha upendo kwa watoto wao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kuwapa mahitaji muhimu kama chakula, mavazi, malazi na elimu. Pia wanapaswa kuwasikiliza, kuwashauri na kuwahimiza kufanya mambo mema. Mtoto anapopata upendo kutoka kwa wazazi wake hujenga kujiamini na kuwa na tabia nzuri.

Walimu nao wana nafasi muhimu katika kuonesha upendo kwa watoto shuleni. Wanapaswa kuwafundisha kwa uvumilivu, kuwaheshimu na kuwasaidia wanapokutana na changamoto mbalimbali. Hali hii huwafanya watoto wapende kujifunza na kufaulu katika masomo yao.

Kwa upande mwingine jamii nzima ina wajibu wa kuwalinda na kuwajali watoto. Watoto wanapaswa kuishi katika mazingira salama yasiyo na unyanyasaji wala ubaguzi. Wanapopewa upendo na ulinzi hukua wakiwa raia wema wenye mchango mkubwa kwa taifa.

Kwa kumalizia upendo kwa mtoto ni msingi wa malezi bora. Kila mzazi, mlezi, mwalimu na mwanajamii anapaswa kuhakikisha kuwa mtoto anapata upendo unaostahili ili akue na kuwa mtu mwema na mwenye mafanikio katika maisha yake.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments