Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika jamii zetu majukumu ya malezi ya watoto yamekuwa yakihusishwa zaidi na wanawake lakini leo tunaona wanaume wengi wakishiriki katika malezi ikiwa ni pamoja na kubeba watoto. Swali la msingi ni je kitendo hiki ni ishara ya mapenzi au ni utumwa kwa mwanaume?
Kwanza kabisa kubeba mtoto kwa mwanaume kunaweza kuonekana kama mapenzi na uwajibikaji wa kifamilia. Mwanaume anapombeba mtoto wake anamwonesha upendo, huruma na kujali. Hii ni njia ya kuimarisha uhusiano kati ya baba na mtoto. Pia inaonesha kuwa mwanaume anashiriki kikamilifu katika malezi badala ya kuyaacha yote kwa mama. Hali hii huleta mshikamano na furaha ndani ya familia.
Katika upande mwingine baadhi ya watu huona kubeba mtoto kama mzigo au utumwa hasa kama mwanaume analazimishwa kufanya hivyo bila hiari au bila kugawana majukumu kwa usawa. Ikiwa majukumu ya malezi yanawekwa upande mmoja tu bila makubaliano inaweza kusababisha uchovu na hisia za kunyonywa. Hali hii inaweza kuharibu mahusiano ndani ya familia.
Hata hivyo ukweli ni kwamba malezi ya mtoto si utumwa bali ni jukumu la wazazi wote wawili. Kinachohitajika ni mawasiliano mazuri na kugawana majukumu kwa heshima na upendo. Mwanaume anaposhiriki katika malezi kwa hiari anakuwa akionesha ukomavu na upendo wa kweli.
Kubeba mtoto na kushiriki katika malezi kwa ujumla si utumwa bali ni mapenzi na uwajibikaji endapo kunafanyika kwa makubaliano na upendo. Utumwa hujitokeza pale tu ambapo hakuna usawa na heshima katika kugawana majukumu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment