JE! KATUNI NI WALIMU WAPYA KWA MAADILI YA WATOTO?

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Katuni ni moja ya aina za burudani ambazo hupendwa sana na watoto. Watoto wengi hutumia muda wao kuangalia katuni kwenye televisheni, simu au kompyuta. Katuni hutengenezwa kwa lengo la kuburudisha, kufundisha na kuwapa watoto mafunzo mbalimbali ya maisha. Kutokana na hali hiyo katuni zina mchango mkubwa katika kujenga maadili ya watoto iwapo zitachaguliwa na kutumiwa kwa usahihi.

Katuni huwafundisha watoto tabia njema kama vile uaminifu, heshima na upendo. Katika katuni nyingi wahusika wakuu huoneshwa wakisema ukweli, kusaidiana na kuheshimu watu wengine. Watoto wanapoangalia matendo hayo mara kwa mara hujifunza kuyaiga katika maisha yao ya kila siku.

Aidha katuni zinaweza kuwafundisha watoto umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa. Wahusika wengi wa katuni hukutana na changamoto mbalimbali lakini huendelea kupambana hadi kufikia malengo yao. Mafunzo haya huwasaidia watoto kujenga tabia ya uvumilivu na kujituma katika masomo na shughuli nyingine.

Hata hivyo si katuni zote zina mchango mzuri katika kujenga maadili. Baadhi ya katuni huonesha vurugu, lugha mbaya au tabia zisizofaa kwa watoto. Watoto wanaoweza kuiga matendo hayo wanaweza kuathirika kitabia. Hivyo wazazi na walezi wanapaswa kusimamia aina ya katuni wanazoangalia watoto ili kuhakikisha zinawajenga badala ya kuwaharibu.

emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments