Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Siku moja nilikutana na mtu njiani aliyekuwa na shida ndogo. Labda alipotea njia au alihitaji msaada kidogo tu.Sikuwa na sababu ya kumsaidia… lakini nilifanya tu kwa moyo.
Baada ya hapo maisha yaliendelea kawaida. Nililisahau kabisa tukio lile.
Miaka ilipita.Siku moja nilijikuta kwenye hali ngumu sana. Nilihitaji msaada na sikuwa najua nitapata wapi.Nilihisi peke yangu.
Lakini ghafla mtu mmoja akajitokeza kunisaidia.Tulipoanza kuzungumza vizuri ndipo nikamtambua.Alikuwa yule yule niliyemsaidia zamani.
Aliniangalia na kusema“Sikuwahi kusahau ulichonifanyia.”
Nilibaki kimya nikiwa na mshangao na shukrani kwa wakati mmoja.
Baada ya hapo nilijifunza vitu vingi katika maisha tunayoishi inabidi kupendana na kuishi kwa kujaliana na kuchukuliana kwa mapungufu kwani hakuna mtu anaye ijua kesho yake isipokua Mungu mwenyewe.
Emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment