UMUHIMU WA WATOTO KUJIFUNZA UWAZI NA KUONGEA UKWELI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Watoto wengi hukua wakihisi kuwa kusema ukweli wakati mwingine kunaweza kuwa vigumu. Wengine huogopa kukemewa, kuadhibiwa au kuchekwa na wenzao. Lakini ukweli ni kwamba kuongea ukweli ni moja ya tabia muhimu sana ambayo kila mtoto anapaswa kujifunza mapema maishani.

Kwanza kabisa kusema ukweli huwasaidia watoto kujenga uaminifu. Mtu anaposema ukweli mara kwa mara, wazazi, walimu na marafiki huanza kumwamini zaidi. Uaminifu huu husaidia mtoto kupata nafasi nzuri shuleni na hata katika jamii.

Kusema ukweli humfanya mtoto kuwa na moyo mwepesi. Mtoto anayesema uongo mara nyingi huishi kwa hofu kwamba atagunduliwa. Hii inaweza kumfanya awe na wasiwasi muda wote. Lakini mtoto anayesema ukweli huishi kwa amani ya moyo.

Shuleni watoto hukutana na changamoto nyingi kama mitihani. Wakati mwingine mtoto anaweza kushindwa kufanya kazi au kupata alama ndogo.

Kwa mfano kama mtoto amevunja kitu au amefanya kosa kusema ukweli ni bora kuliko kuficha. Makosa yanapotokea yanaweza kurekebishwa bila matatizo makubwa zaidi.

Kusema ukweli si jambo rahisi kila wakati lakini ni tabia inayojenga maisha bora. Watoto wanapojifunza kuwa waaminifu tangu wakiwa wadogo wanakuwa watu wazima wenye maadili mazuri na wanaoheshimika katika jamii.

Emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments