Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Kulikuwa na mtoto mmoja aliyependa sana kucheza na simu ya mama yake. Kila siku akitoka shule badala ya kufanya kazi za nyumbani au kusoma alikuwa akikaa na simu akiangalia video na kucheza michezo.
Mwanzoni mama yake hakumkataza sana. Lakini taratibu mtoto alianza kubadilika. Hakupenda tena kucheza nje na marafiki zake, hakumaliza kazi za shule na hata usingizi ulikuwa unampata darasani.
Siku moja mwalimu alimpa kazi ya kusoma hadithi mbele ya darasa. Aliposimama alishindwa kusoma vizuri kwa sababu alikuwa hajafanya mazoezi ya kusoma kwa muda mrefu.
Wanafunzi wengine wakacheka kidogo. Mtoto alihuzunika sana.
Aliporudi nyumbani alikaa kimya. Mama yake akamuuliza: “Kuna nini?”
Mtoto akasema “Nimegundua simu imenifanya nisipende kusoma tena".
Mama yake hakumfokea. Badala yake walikubaliana muda maalum wa kutumia simu na muda wa kusoma.
Baada ya wiki chache mtoto alianza kubadilika. Alifanya vizuri darasani akarudi kucheza na marafiki zake na akawa mwenye furaha zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment