Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mwanzoni haikuwa tatizo kubwa.Nilikuwa nachukua simu yangu kidogo tu kuangalia video, status au kucheki marafiki. Ilikuwa kama burudani ya kawaida.
Lakini polepole kitu kidogo kikawa kikubwa.
Dakika 10 zikawa saa moja.Saa moja zikawa masaa matatu.
Nilianza kupoteza muda wa kusoma bila hata kugundua. Kila nikijaribu kusoma nilikuwa napata tamaa ya kushika simu tena.
Nilijipa ahadi nyingi “Nitasoma baadaye…”
“Leo ngoja nipumzike…”Lakini baadaye haikuwahi kufika.
Mtihani ulipokaribia nilianza kupata hofu kidogo lakini tayari ilikuwa imechelewa.
Siku ya mtihani nilikaa darasani nikiangalia karatasi ya maswali kama mgeni. Mambo mengi sikuyaelewa. Nilijua tayari nimeharibu.
Matokeo yalipotoka ilikuwa ni pigo kubwa sana kwangu. Nilifeli vibaya.
Siku hiyo nilikaa peke yangu nikitafakari kila kitu. Nilijiuliza: “Tatizo lilikuwa nini?”
Jibu lilikuwa wazi matumizi mabaya ya simu.
Nilifanya uamuzi mgumu Nikaweka mipaka.
Nilipunguza muda wa kutumia simu nikaanza kupanga ratiba ya kusoma. Haikuwa rahisi mwanzoni lakini nilijilazimisha.Baada ya muda nilianza kuona mabadiliko.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment