Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Nilikuwa na marafiki wengi sana. Tulikuwa tunacheka pamoja, tunatoka pamoja na kila mtu alionekana kuwa karibu sana na mimi.
Nilihisi nina bahati kuwa na watu wengi pembeni yangu na wanao nitakia mema katika maisha yangu.Lakini siku moja maisha yalibadilika ghafla.
Nilipata shida kubwa ambayo ilinifanya nihitaji msaada wa watu wangu wa karibu.
Nilianza kuwapigia simu…Mmoja hakupokea.
Mwingine alisema yuko busy na hawezi kuwa na mimi karibu muda huu.
Mwingine aliahidi kuja lakini hakutokea.Kadri muda ulivyopita ndivyo nilivyoanza kuona ukweli.
Wale wote niliowaona kama “marafiki wa karibu”… walipotea.
Nilibaki peke yangu.Lakini kuna mtu mmoja tu ambaye hata sikuwa namchukulia sana ndiye alikuja. Hakuniuliza maswali mengi. Hakunihukumu. Alikaa na mimi, alinisaidia na alinipa moyo.
Emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment