Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Kwa muda mrefu, niliona familia kama kero.
Nilikuwa napenda kuwa nje zaidi na marafiki kwenye michezo au mahali popote mbali na nyumbani.Niliona kama nyumbani kuna masharti mengi: maswali, maelekezo na kukumbushwa mambo.Nilihisi uhuru uko nje.
Sikujua kuwa nilikuwa napuuza kitu muhimu sana.
Siku moja nilikumbana na changamoto kubwa. Ilikuwa ni hali ambayo ilinifanya nihitaji msaada wa haraka.Nilifikiria marafiki wangu watanisaidia.
Lakini mambo hayakuwa hivyo. Wengine walikuwa busy.
Wengine hawakujali sana.Nilijikuta nikiwa peke yangu.
Mwisho nilirudi nyumbani.Nilikuwa na hofu sijui nitapokelewa vipi baada ya muda wote niliokuwa najitenga.Lakini kilichotokea kilinishangaza.
Familia yangu ilinipokea kwa upendo mkubwa. Hakuna aliyenihukumu. Walinisikiliza, walinisaidia na walinisimamia mpaka nikasimama tena.
Nilihisi kitu ambacho sikuwa nimehisi kwa muda mrefu usalama.
Ndipo nilipotambua kuwa nilikuwa napuuza sehemu muhimu zaidi ya maisha yangu.
Kuanzia hapo nilianza kuthamini familia yangu zaidi.
Emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment