NIDHAMU SHULENI NI UFUNGUO WA MAFANIKIO YA MTOTO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids.com

Shule ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mtoto. Hapo ndipo watoto hujifunza kusoma, kuandika na pia kujifunza tabia nzuri za maisha. Lakini ili mtoto afanikiwe shuleni kitu kimoja cha msingi kinahitajika sana nidhamu.

Nidhamu ni uwezo wa mtoto kujiongoza, kufuata sheria na kufanya kile kinachotakiwa kwa wakati unaofaa.

Kwanza nidhamu humsaidia mtoto kufanikiwa masomoni. Mtoto anayesikiliza darasani na kufanya mazoezi ya masomo hupata uelewa mzuri zaidi.

Pili nidhamu humfundisha mtoto uwajibikaji. Anajua kile anachopaswa kufanya bila kusubiri kukumbushwa kila wakati.

Tatu nidhamu humsaidia mtoto kuwa na heshima kwa wengine. Hii inajenga mahusiano mazuri kati yake, walimu na wanafunzi wenzake.

Mtoto asiye na nidhamu anaweza kukumbana na matatizo kama: Kushindwa masomo, Kukemewa mara kwa mara, Kupoteza marafiki wazuri, Kutokuwa na mpangilio mzuri wa maisha

Nidhamu haiji kwa siku moja. Inajengwa hatua kwa hatua kwa kusikiliza ushauri wa wazazi na walimu, Kufanya ratiba ya masomo na kuifuata na Kujifunza kujitawala (self-control)

Nidhamu ni msingi wa mafanikio ya mtoto shuleni na maishani kwa ujumla. Mtoto mwenye nidhamu hujenga maisha bora ya baadaye yenye mafanikio na heshima.

emakulatamsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments