Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Usiku mmoja wa mvua kubwa radi zilikuwa zinapasua anga la kijiji cha Mwikatsi. Watoto wote walikuwa wamejificha majumbani mwao isipokuwa mmoja tu mtoto aitwaye Tunu.
Tunu alikuwa maarufu kijijini kwa kujifanya anajua kila kitu. Ukisema nyota yeye anasema anazijua. Ukisema simba yeye anasema aliwahi kupigana naye msituni. Hata wazee walimwita kwa siri “Mtoto Mjuaji.”
Siku hiyo bibi mmoja mzee mwenye fimbo ya ajabu alifika kijijini. Alivaa joho jeusi na macho yake yalionekana kung’aa kama moto.Aliwaambia wanakijiji.
“Ndani ya msitu wa Kiza kuna sanduku la siri. Atakayelifungua atapata hekima kubwa kuliko dhahabu.” Watu wote waliogopa kwenda huko. Lakini Tunu akacheka.
“Hilo ni jambo rahisi! Mimi najua kila njia ya msituni.” Asubuhi iliyofuata akaingia msitu wa Kiza akiwa peke yake. Kadiri alivyozidi kutembea miti ilianza kutoa sauti za ajabu.
“Rudi… rudi…”Lakini Tunu hakusikia.Ghafla akafika kwenye daraja la zamani lililotikisika juu ya mto mweusi. Katikati ya daraja alikutana na ndege mkubwa mwenye macho mekundu.
Ndege akasema kwa sauti nzito “Kabla hujavuka jibu swali langu. Ukikose hutoki hapa.”
Tunu akameza mate lakini akajifanya jasiri.
Tunu akashangaa. Akaendelea mbele mpaka alipofika kwenye sanduku la siri. Alipolifungua, hakukuwa na dhahabu wala almasi. Kulikuwa na kioo tu.
Kwenye kioo kulikuwa na maneno “Mwenye kujua kila kitu hafundishiki. Mwenye kuuliza huongezeka hekima” Tunu alikaa kimya kwa muda mrefu. Alipojirudi kijijini alikuwa tofauti kabisa. Akaanza kusikiliza watu, kuuliza maswali na kusaidia wengine badala ya kujisifu.
Na tangu siku hiyo kijiji cha Mwikatsi hakikumwita tena “Mtoto Mjuaji kilimwita mtoto Mwenye Hekima.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment