Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika jiji la Dar es Salaam aliishi mtoto mmoja aitwaye Kelvin. Kelvin alipenda sana michezo ya simu kuliko masomo. Kila siku baada ya shule alienda kwenye kibanda cha michezo badala ya kurudi nyumbani kufanya kazi za shule.
Mama yake alikuwa akimwonya kila mara “Kelvin ukizoea kutangatanga mjini usiku na kucheza michezo kila siku utaharibu maisha yako.”
Lakini Kelvin hakusikia. Aliona maisha ya mjini ni ya starehe tu.
Siku moja Kelvin alipewa pesa ya kununua vitabu vya shule. Badala ya kununua vitabu alienda kucheza michezo ya video na kula chipsi na marafiki zake. Aliporudi nyumbani alimdanganya mama yake kuwa pesa zimepotea.
Baada ya wiki chache mitihani ilifika. Wanafunzi wengi walifaulu kwa sababu walikuwa wakijisomea. Kelvin hakufaulu hata somo moja. Aliona aibu sana mbele ya walimu na wazazi wake. Siku hiyo baba yake alimwita na kusema.
“Mji una vitu vingi vizuri na vibaya. Ukikosa nidhamu maisha ya mjini yanaweza kukupoteza.”
Kelvin alilia na kuahidi kubadilika. Akaanza kutumia muda wake vizuri kusoma na kusaidia wazazi wake nyumbani.
Miaka ilipopita Kelvin alifaulu masomo yake na kuwa mhandisi maarufu jijini.
Mafunzo: Maisha ya mjini yanahitaji nidhamu na matumizi mazuri ya muda ili kufanikiwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment