Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Zawadi na Amina walikuwa marafiki wakubwa sana tangu darasa la kwanza. Walikaa pamoja darasani, walicheza pamoja na walisaidiana kwenye masomo.
Siku moja mwanafunzi mpya aitwaye Diana alihamia darasani kwao. Diana alikuwa mtulivu sana na hakujua mtu yeyote.
Baadhi ya wanafunzi walianza kumtenga na kumcheka kwa sababu alikuwa mnyonge na mwenye aibu. Amina aliona hali ile lakini aliogopa kusema chochote ili asije naye akaanza kuchekwa.Lakini Zawadi alichukua hatua. Alimkaribia Diana na kumwambia,
“Usijali unaweza kukaa nasi.” Diana alifurahi sana. Taratibu alianza kuzoea mazingira na hata kuanza kufanya vizuri darasani.
Siku moja mwalimu aliwaweka wanafunzi kwenye vikundi vya kazi. Kikundi cha Zawadi kilifanya vizuri sana hasa kwa sababu Diana alikuwa mzuri katika masomo.
Baada ya hapo wanafunzi waliokuwa wanamcheka waligundua kosa lao na wakaanza kumheshimu.Amina alimwambia Zawadi
“Ulikuwa sahihi kumsaidia. Mimi niliogopa tu.”
Zawadi akasema“Kufanya jambo sahihi ni muhimu kuliko kuogopa watu.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment