"UKWELI ULIOKUJA BAADA YA RECORD KUZIMA"

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na marafiki wawili Neema na Brian waliokuwa wanaishi mjini. Wote walipenda sana simu zao na kutumia TikTok na WhatsApp kila siku baada ya shule.

Siku moja walipokuwa wanarudi nyumbani walimuona mtoto mdogo akiwa pembeni ya barabara akilia. Watu wengi walikuwa wanapita lakini hakuna aliyemsikiliza kila mtu alikuwa bize na simu zake.

Brian alisema “Labda nimrekodi nimuweke TikTok inaweza kupata views nyingi.”

Neema akamwangalia na kusema “Hapana huyu anahitaji msaada siyo video.”

Walimsogelea yule mtoto na kumuuliza kulikoni. Mtoto alisema amepotea na haijui njia ya kwenda nyumbani. Neema akatumia simu yake kumpigia mama yake kupitia WhatsApp baada ya mtoto kutoa namba.

Baada ya muda mfupi mama yake alifika akiwa na wasiwasi mkubwa. Alipomuona mtoto wake alifurahi sana na kuwashukuru Neema na Brian.

Brian alihisi aibu kidogo na kusema “Leo nimejifunza kitu… si kila kitu ni content.”

Neema akatabasamu “Ndiyo wakati mwingine msaada ni muhimu kuliko likes.”

Kuanzia siku hiyo Brian alianza kutumia mitandao ya kijamii kwa njia nzuri zaidi si kwa kujifurahisha tu bali pia kusaidia wengine.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments