UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na msichana mdogo aitwaye Aisha. Familia yake ilikuwa haiwezi kumnunulia simu mpya au kutembelea maeneo ya burudani kama wenzake shuleni. Kila siku Aisha alirudi nyumbani baada ya shule akiwa na hisia mchanganyiko hamu ya kucheza na rafiki zake lakini hofu ya kutotimiza matarajio.

Siku moja shuleni walipokuwa wakijifunza kuhusu mradi wa kijamii walimu waliwaagiza wanafunzi kuangalia changamoto za jamii zao na kujaribu kuleta suluhisho. Wazazi wa Aisha hawakuwa na pesa ya kusaidia mradi wowote wa kifahari.

Lakini Aisha hakukata tamaa. Aliona changamoto ya maji safi kwa jirani yao mdogo na akatengeneza wazo la kipekee kutumia mabaki ya plastiki na maboksi ya karatasi kutengeneza mifumo midogo ya kuchuja maji safi.

Aisha alifanya kazi kwa bidii pamoja na rafiki yake wakikusanya vifaa vya bure kutoka nyumba zao na mtaa. Wakati wa kuonesha mradi kwa walimu na wanafunzi wenzake kila mtu alishangaa na kupongeza ubunifu wake.

Aligundua kuwa ingawa hakuwa na simu mpya au vifaa vya gharama kubwa alibadilisha changamoto kuwa suluhisho la kweli.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments