TEKNOLOJIA NI NZURI LAKINI LAZIMA ITUMIKE KWA NIDHAMU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kelvin alikuwa mvulana wa darasa la saba. Siku moja baba yake alimwachia simu ili aitumie kujifunzia masomo mtandaoni.

Mwanzoni Kelvin alifuata maelekezo. Alitazama video za masomo na kufanya mazoezi. Lakini baada ya muda alianza kutumia simu kucheza michezo na kuangalia video zisizo za masomo.

Kila siku alipoulizwa na baba yake alisema “Ndiyo baba ninajifunza.”

Lakini matokeo yake shuleni yalianza kushuka. Mwalimu alimwita na kumwambia

“Kelvin ulikuwa unafanya vizuri kuna nini kimebadilika?”

Kelvin hakujibu. Alijisikia vibaya moyoni.

Siku moja baba yake alipoangalia simu aligundua kuwa Kelvin alikuwa hatumii muda mwingi kujifunza kama alivyosema. Baba yake hakupiga kelele bali alimwita na kuzungumza naye kwa utulivu. “Mwanangu simu siyo mbaya lakini matumizi yake yanaweza kuharibu au kujenga maisha yako.”

Maneno yale yalimgusa Kelvin sana. Aligundua kosa lake na akaamua kubadilika. Alianza kupanga muda wake vizuri wakati wa masomo na wakati wa kupumzika.

Baada ya mudabmatokeo yake yakaanza kuimarika tena.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments