SAFARI YA ASUBUHI YA JOHN

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

John alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita aliyekuwa na tabia ya kuchelewa kuamka. Kila siku mama yake alimwamsha mara nyingi kabla hajaamka kweli.

Siku moja mama yake alimwambia “John kesho sitaweza kukuamsha jitahidi kuamka mwenyewe.”

Usiku ule John alijiambia “Nitaamka mapema kesho.” Lakini hakupanga vizuri vitu vyake vya shule.

Asubuhi ilipofika alizima saa ya kengele na akaendelea kulala. Alipoamka tena ilikuwa tayari amechelewa sana!

Alikimbia haraka kujiandaa lakini alipofika shuleni tayari kipindi cha kwanza kilikuwa kimeanza. Mwalimu alimruhusu kuingia lakini alimwonya.

Baada ya shule John alijisikia vibaya. Aligundua kuwa kuchelewa kwake kulikuwa tatizo lake mwenyewe si la mama yake. Siku iliyofuata aliweka saa ya kengele mapema na akaamka mara moja. Alijiandaa kwa utulivu na akafika shule kabla ya muda.

Mwalimu alipomwona alitabasamu na kusema

“Hivyo ndivyo inavyotakiwa.”

John alifurahi na akaamua kuendelea na tabia hiyo nzuri.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments