MAFANIKIO YANATOKANA NA BIDII, SI MIUJIZA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Katika mji mdogo wa Kijani aliishi mvulana aitwaye Samir. Samir hakuwa anapenda kusoma vitabu hata kidogo. Kila alipopewa kazi ya kusoma alikuwa akisema “Hii ni ngumu siipendi.”

Siku moja akiwa anasaidia kusafisha maktaba ya shule alikuta kitabu cha zamani sana kikiwa kimefichwa nyuma ya rafu. Kitabu kile kilikuwa na jalada la ngozi na kilionekana cha ajabu.

Alipokigusa ghafla kilifunguka chenyewe! Sauti ya ajabu ilisikika “Hatimaye umeamka mimi.”

Samir aliruka nyuma kwa hofu. “Nani huyo?!”“Mimi ni Kitabu cha Maarifa kilijibu kwa sauti tulivu".

Samir alishangaa sana. “Kitabu kinawezaje kuongea?”“Kwa wale wasiotaka kujifunza mimi nipo kimya. Kwa wanaotaka kujua nafunguka na kuzungumza” kitabu kilisema.

Samir alikuwa na hofu lakini pia na hamu. “Unaweza kunionesha kitu?”

Kitabu kilifunguka kurasa zake zenye mwanga na kumwonrsha picha za milima, sayansi na historia. “Maarifa yanafungua milango mingi maishani". kilisema. Kuanzia siku hiyo Samir alianza kukitembelea kitabu kila siku kwa siri. Kila alipokisoma alijikuta anaelewa mambo haraka zaidi. Lakini kulikuwa na tatizo Samir bado alikuwa mvivu darasani. Hakufanya kazi zake na matokeo yake yakaanza kushuka.

Kitabu kilimwambia “Kusoma bila kufanya bidii ni kama mbegu bila maji.”

Samir hakuelewa vizuri mwanzoni. Siku ya mtihani mkubwa ilipofika alijaribu kukumbuka kile alichosoma. Lakini kwa sababu hakujifunza kwa bidii alisahau mengi.

Alitoka mtihani akiwa na huzuni Usiku ule kitabu kilimwita tena.

“Leo umeelewa nini?”Samir alisema kwa sauti ya chini “Nimekosa kwa sababu nilikuwa mvivu.” Kitabu kilifungua kurasa za mwisho zikionesha picha ya mvulana aliyefanikiwa kwa bidii na uvumilivu.“Kujifunza ni safari si tukio moja” kilisema. Kuanzia siku hiyo Samir alibadilika kabisa. Alianza kusoma kwa bidii kufanya mazoezi, na kuuliza maswali darasani.Baada ya muda alikua mmoja wa wanafunzi bora shuleni.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments