Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hamisi alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano aliyeishi na shangazi yake mjini. Alikuwa mvulana mchangamfu lakini alikuwa na tabia ya kupenda vitu vya haraka haraka bila kufikiri sana.
Siku moja shuleni walipewa kazi ya kikundi kufanya mradi kuhusu “Usafi wa Mazingira.” Kila kikundi kilitakiwa kupanga, kuchora na kuandika ripoti.
Katika kikundi cha Hamisi kila mtu alipewa jukumu. Hamisi alipewa jukumu la kuandika ripoti kwa sababu alikuwa na mwandiko mzuri.
Lakini badala ya kufanya kazi Hamisi alicheza na marafiki zake baada ya shule. Alijiambia
“Nitafanya kesho bado kuna muda.” Siku ziliendelea kupita bila kufanya kazi. Wenzake walimaliza sehemu zao lakini Hamisi alikuwa bado hajaanza.
Siku ya kuwasilisha mradi ilipofika kikundi kilikusanyika haraka. Waligundua kuwa ripoti haipo.
Mwalimu aliuliza“Ripoti yenu iko wapi?” Wote wakanyamaza kimya. Hamisi alihisi aibu kubwa. Wenzake walimwangalia kwa huzuni kwa sababu kazi yao ilionekana haitakamilika.
Mwalimu aliwaambia “Kazi ya kikundi inahitaji uwajibikaji wa kila mmoja kukosa sehemu moja kunaathiri wote.”Baada ya somo Hamisi alimwambia mwalimu ukweli wote. Alikiri kuwa alichelewesha kazi.
Mwalimu hakumkemea sana lakini alimwambia kwa upole “Kosa ni sehemu ya kujifunza lakini muhimu ni kubadilika.”
Kikundi kiliruhusiwa kurekebisha mradi kwa muda wa ziada. Hamisi alifanya kazi kwa bidii usiku mzima akisaidiana na wenzake.
Baada ya kuwasilisha tena mradi wao ulikuwa mzuri. Lakini Hamisi hakusahau somo alilojifunza.
Kuanzia siku hiyo alianza kufanya kazi mapema na kuwajibika zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment