Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Asha alikuwa msichana wa darasa la tano aliyependa sana kusoma. Kila siku alienda shule mapema akiwa na daftari lake safi na kalamu nzuri.
Siku moja alipofika darasani aligundua kuwa daftari lake la hesabu halipo. Alitafuta kwenye begi lake mara nyingi lakini hakuliona. Alianza kuwa na wasiwasi sana.
Rafiki yake Mariam alimwuliza “Asha kuna nini?”
Asha akajibu “Nimepoteza daftari langu na leo tuna kazi ya mwalimu.”
Muda wa somo ulipofika mwalimu aliingia darasani na kuanza kukagua madaftari. Asha alisimama kimya akiwa na huzuni. Kabla hajazungumza mtoto mmoja aitwaye Juma alisimama na kusema
“Mwalimu jana nilikuta daftari chini ya dawati. Nilienda nalo nyumbani bila kujua ni la nani. Leo nimeleta.”
Alipolitoa Asha alitambua mara moja kuwa ni lake. Alifurahi sana!
“Asante sana Juma!” alisema kwa tabasamu.
Mwalimu alimpongeza Juma kwa uaminifu wake na akawaambia wanafunzi wote
“Uaminifu ni jambo muhimu sana maishani.”
Asha alijifunza kuwa makini na vitu vyake na pia alifurahia kuona kuwa bado kuna watu waaminifu kama Juma.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment