Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana aitwaye Zawadi aliyependa sana kupiga picha na kurekodi video kwa ajili ya Instagram. Kila siku alikuwa anapanga mavazi anatafuta sehemu nzuri na kupost picha ili kupata likes nyingi.
Siku moja aliona msichana mwenzake shuleni Rehema akiwa amekaa peke yake. Wanafunzi wengine walikuwa wanamcheka kwa sababu hakuwa na simu nzuri kama wao.
Zawadi alifikiria “Hii inaweza kuwa video ya kusikitisha watu watapenda…”
Akaanza kurekodi kwa siri ili apate content ya kuweka Instagram.
Lakini ghafla akasimama. Akajiuliza “Je hii ni sawa kweli?”
Badala ya kurekodi alisogea kwa Rehema na kukaa naye. Akaanza kuzungumza naye na kumfariji. Baadaye alimsaidia kujiunga na kikundi cha wanafunzi wengine waliokuwa wema.
Baada ya siku chache Rehema alianza kufurahi tena na kupata marafiki.
Rafiki wa Zawadi alimuuliza “Mbona hukupost ile video? Ilikuwa ingeenda viral!”
Zawadi akatabasamu na kusema “Sio kila kitu kinapaswa kuwa content… wengine wanahitaji upendo si camera.”
Tangu siku hiyo Zawadi alianza kutumia Instagram kuhamasisha watu kufanya mema siyo kuonesha matatizo ya wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment