REHEMA NA DARASA LA SANAA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Rehema alikuwa mwanafunzi mdogo aliyeenda shule ya msingi. Siku moja mwalimu wao aliwapa darasa la kuchora. Wanafunzi walifurahia sana lkini Rehema alihisi hakuwa mzuri sana katika kuchora.

Alijaribu kuchora mti ulikua mbaya sana haukuwa sawa kama alivyotarajia. Alijisikia huzuni na alitaka kuacha kuchora kwasababu alijua hawezi kuwa bora.

Mwalimu alikuja karibu na kumwambia,

“Rehema siio lazima uwe bora kwa mara moja. Muhimu ni kujaribu na kufurahia kile unachochora.”

Rehema alirudi mezani akajaribu tena na alikamilisha mchoro wake. Wanafunzi wenzake walimpongeza kwa bidii yake. Alijifunza kuwa kujaribu na kushikilia jambo ni muhimu zaidi kuliko kuwa bora mara moja.

Tangu siku hiyo Rehema alipenda kuchora vitu mbalimbali anavyoviona mbele yake na akiwa nyumbani ametulia alichukua daftari lake la kuchezea na kuanza kuchora vitu mbalimbali na akazidi kuwa bora zaidi na zaidi.Na pia alijunza kuwa kila kitu kinahitaji mazoezi ya mara kwa mara

emakulatemsafiri@gmail.com

0753903872



0/Post a Comment/Comments