Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika kijiji kidogo kilichojaa mashamba ya mahindi, aliishi mvulana aitwaye Beny. Beny alikuwa mtoto mchangamfu na mwenye ndoto kubwa. Alipenda sana kuchora picha za wanyama na magari.
Siku moja shule yao ilitangaza mashindano ya kuchora. Mshindi angepewa zawadi ya daftari jipya na rangi za kuchorea. Beny alifurahi sana lakini baadaye akaanza kuogopa. Aliwaza “Je,kama nitachora vibaya? Je kama wengine watanicheka?”
Alipofika nyumbani alimwambia mama yake “Naogopa kushiriki mashindano.”
Mama yake akamwambia kwa upole “Beny muhimu si kushinda. Muhimu ni kujaribu na kuonesha kipaji chako.”
Maneno yale yakampa Beny nguvu. Kesho yake alikaa chini ya mti na kuanza kuchora simba mkubwa akiwa porini. Alitumia rangi kwa makini na kwa moyo wote.
Siku ya kutangaza mshindi ilipofika Beny hakushinda nafasi ya kwanza. Lakini mwalimu alimuita mbele na kusema “Beny umeonesha juhudi na ubunifu mkubwa sana.”
Wanafunzi walimpigia makofi na Beny alitabasamu kwa furaha. Aligundua kuwa kujiamini na kujaribu ni ushindi wenyewe.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment