UAMINIFU NI HAZINA KUBWA KULIKO MALI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Hapo zamani kidogo katika jiji kubwa la Dar es Salaam waliishi watoto wawili waliokuwa marafiki wakubwa sana Neema na Kelvin. Waliishi katika mtaa wenye magari mengi, maduka na majengo marefu.

Siku moja baada ya kutoka shuleni walikuwa wakitembea kando ya barabara wakielekea nyumbani. Ghafla Neema aliona simu nzuri ya mkononi imeanguka karibu na kituo cha daladala.

“Kelvin angalia! Kuna simu hapa chini” Neema alisema.

Kelvin akaichukua na kusema “Ni simu ya bei ghali sana. Tunaweza kuiuza tupate pesa.”

Neema akatikisa kichwa “Si vizuri kuchukua kitu kisicho chetu. Lazima kuna mtu ana huzuni sasa hivi akiitafuta.”

Wakaamua kukaa karibu na pale pale wakisubiri mwenye simu. Baada ya muda mfupi dada mmoja alikuja huku akitazama chini kwa wasiwasi.

“Samahani watoto je mmeona simu yangu? Nimeipoteza hapa” aliuliza kwa sauti ya huzuni.

Neema akatabasamu na kusema, “Ndiyo dada tumeiona. Hii hapa.”

Yule dada alifurahi sana na kuwashukuru. Aliwaambia “Asanteni kwa uaminifu wenu. Si kila mtu angefanya hivi.”

Watoto walirudi nyumbani wakiwa na furaha kubwa mioyoni mwao. Walijivunia kufanya jambo jema katikati ya jiji lenye watu wengi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments